Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 22, 2025 Local time: 12:23

Serikali ya Malawi yafungia  vituo vitatu vya televisheni na sita vya radio


Rais wa Malawi Lazarus Chakwera akiwasili Addis Ababa Februari 5, 2022 kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa Kikao cha 35 cha Umoja wa Afrika. REUTERS.
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera akiwasili Addis Ababa Februari 5, 2022 kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa Kikao cha 35 cha Umoja wa Afrika. REUTERS.

Serikali ya Malawi imefunga  vituo vitatu vya televisheni na vituo sita vya radio kwa kushindwa  kulipa ada ya mwaka ya leseni. Mamlaka ya vyombo vya habari nchini humo  inatarajiwa kufuta leseni za vyombo vya habari mpaka 30 ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Serikali ya Malawi imefunga vituo vitatu vya televisheni na vituo sita vya radio kwa kushindwa kulipa ada ya mwaka ya leseni. Mamlaka ya vyombo vya habari nchini humo inatarajiwa kufuta leseni za vyombo vya habari mpaka 30 ifikapo mwisho wa mwaka huu. Kundi la utetezi la ndani linasema hatua hii si njia muafaka na ya haki.

Mandy Pondani makamu mwenyekiti wa Taasisi ya Habari kwa Kusini mwa Afrika nchini Malawi. Ameiambia VOA kwamba kkufungwa kwa vyombo vya habari kutapunguza mwanya wa habari na kuondoa uhuru na mafanikio ya kidemokrasia yaliyopatikana katika muda wa miaka 30 iliyopita.

Anasema Mamlaka ya Kusimamia Mawasiliano nchini Malawi au MACRA, ni vyema ifikirie athari za kiuchumi kwa kufunga vyombo hivyo.

“Tunauangalia uchumi ambao haufanyi kazi vizuri. Unaweza kukubaliana na mimi kwamba nchini Malawi hivi sasa karibu kila biashara imeathiriwa. Kwa hakika taasisi za habari hazikuwa zinajitegenezea fedha. Sisi pia tunatoka kwenye janga ambalo limefunga taasisi zote. Kwahiyo, tulidhani pengine MACRAingefikiria vya kutosha masuala kama hayo,” amesema Pondani.

Vyombo vya habari ambavyo vimekumbwa na hatua hii ni Rainbow Televisheni, Angaliba Televisheni, Ufulu Televisheni, Angaliba FM, Capital Radio, Sapitwa FM, Joy Radio, Ufulu FM na Galaxy FM.

Taarifa za karibuni kutoka MACRA zinaonyesha kwa jumla, leseni za vituo 23 vya radio na sita vya televisheni huenda vikafutiwa leseni zao ifikapo mwisho wa mwaka.

Baadhi ya vituo vimelipa ada zao lakini bado pia vimefungiwa.

Aubrey Kusakala ni meneja wa kituo cha televisheni cha Rainbow, amesema kituo chake kimefungwa licha ya kulipa bili ya dola 10,000.

Anahisi ni suala lenye ushawishi wa kisiasa, “kwasababu tunaangalia jinsi tulivyotendewa. Tulifanya malipo Juni 20. Walichukua malipo yetu miezi miwili baadaye, ikimaanisha kuwa hawakuwa na haja ya fedha. Walikuwa wanataka kutufungia. Baadhi ya habari tulizokusanya kwa hakika zinaonyesha kwamba serikali kupitia MACRA haikuta sisi tuwepo kwenye soko,” ameongezea Kusakala.

Pondani wa MISA-Malawi anasema hilo linatia wasi wasi mkubwa na kusema kile kinachotokea hivi sasa hakielezeki. Katika muda wa miaka zaidi ya 50 ya uhuru wa Malawi, hatujawahi kuona utawala ukifunga vyombo vya habari kama ulivyofanya utawala huu. Inatia dosari na haionyeshi vizuri kwa utawala. Kama ukweli unatakiwa uelezwe kwa kila mtu ili afahamu jukumu la vyombo vya habari ulivyofanya kwa utawala kuwa madarakani. Halafu kufanyiwa vitendo hivi vibaya kwa kweli ssi vizuri na haipendezi.”

MISA-Malawi inasema kufungwa huko kumesababisha kupotea kwa nafasi za ajira 250 ambazo zilikuwa zinashikiliwa na watalaamu wa habari na wafanyakazi wengine na kwamba watu 500 wanatarajiwa kupoteza ajira zao ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Zadziko Mankhambo ni meneja mawasiliano wa MACRA anasema kufungwa kwa vyombo hivyo hakuna uhusiano wowote na uhuru wa habari au siasa. Anasema kuna masuala ambayo yameambatana na leseni zao za utangazaji, ambayo lazima yafuatwe.

Miongoni mwao, anasema, ni kuheshimu ratiba ya malipo.

“Hata. Hivyo, MACRA ni moja ya idada ambazo zinatetea uhuru wa habari. Kwa wakati huu, MACRA inahakikisha kwamba kuna vyombo vya habari vingi zaidi. Na hivi ninavyoongea kuna leseni nyingi ambazo zinasubiri kupata ruhusa ya kurusha matangazo kwa mujibu wa sheria,” amesema Mankhambo.

Mankhambo anasema MACRA haina mipango ya kubadili hatua zake mpaka kuwepo na mabadiliko ya sheria ambayo mamlaka inaziimarisha.

Hata hivyo, MACRA imesema vyombo vya habari ambavyo vimefungwa vinaweza kuomba leseni mpya mara watakapokuwa wamemaliza malipo wanayodaiwa.

XS
SM
MD
LG