Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 19:00

Serikali ya Lebanon yajiuzulu


Aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Haasan Diab.
Aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Haasan Diab.

Waziri mkuu wa Lebanon Hassan Diab, Jumatatu usiku alitangaza kujiuzulu kwa serikali yake, kufuatia shinikizo kutoka kwa raia wa nchi hiyo, ambao wamekuwa wakishiriki maandamano kwa siku kadhaa kufuatia milipuko mikubwa mjini Beirut Jumanne wiki jana, iliyosabisha maafa na hasara kubwa.

Milipuko hiyo ilisababisha vifo vya takriban watu 160 na Zaidi ya elfu tano kujeruhiwa.

Waandamanaji hao wamekuwa pia wakitaka serikali ya Diab kujiuzulu, kwa shutuma za uongozi mbaya na kuhujumu uchumi wa nchi hiyo.

Katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni nchini humo, Diab alisema amechukua hatua hiyo ili kutoa nafasi ya "kuokoa Lebanon," na kuongeza kwamba raia wa nchi hiyo watashiriki katika mchakato huo.

"Mungu isaidie Lebanon," alisema.

Diab aliunde serikali mwezi Januari mwaka huu, baada ya vuta nikuvute ya kisiasa, ambayo hata kabla ya hapo, mara kwa mara ilikuwa ikishuhudiwa nchini humo.

Kabla ya tangazo la kujiuzulu kwa utawala wake Jumatatu, mawaziri na wabunge kadhaa tayari walikuwa wamejiuzulu.

Makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa kulinda usalama yamekuwa yakishuhudiwa tangu Jumamosi.

Milipuko ya Jumanne, ambayo inadaiwa kusababishwa na kemikali aina ya Ammonium Nitrate, inakadiriwa kusababisha hasara ya takriban dola billion tano za Marekani.

XS
SM
MD
LG