Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 19:48

Serikali ya Kenya yaombwa kuwajali vijana


Vijana wengi huingia kwenye makundi ya uhalifu hasa ugaidi kutokana na ukosefu wa ajira
Vijana wengi huingia kwenye makundi ya uhalifu hasa ugaidi kutokana na ukosefu wa ajira

Mhadhiri mmoja wa chuo kikuu cha Pwani nchini Kenya, Profesa Halim Shauri ameikosoa serikali ya Kenya kwa madai ya kushindwa kuangalia maslahi ya vijana hali inayodaiwa kuchangia vijana wengi kujiunga na makundi ya uhalifu pamoja na makundi ya kigaidi.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:01 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Profesa Shauri aliitaka serikali ya Kenya kubuni nafasi za ajira ili kuweza kuwanusuru vijana wenye nia ya kujiunga na makundi hayo ya magenge ya uhalifu uliotukuka. “wengine wamesema kwamba watapea vijana kazi kupitia ile sijui inaitwa NYS, lakini kazi yenyewe iko wapi kwa hivyo ni lazima serikali ijizatiti na iwajibike katika kupeana ajira kwa vijana ili vijana waweze kuacha kushawishiwa kwa kupewa ajira ambazo sio nzuri ambazo zinatuletea balaa extremism na radicalization katika nchi yetu”.

Msomi huyo alishikilia kwamba ni sharti serikali imwangazie kijana ili aweze kujiinua kiuchumi na sio kutumiwa nyakati za kisiasa.

XS
SM
MD
LG