Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 08, 2024 Local time: 17:27

Serikali ya Kenya inapanga kukusanya dola bilioni 1.2 ikirejesha baadhi ya kodi


Bendera ya Kenya
Bendera ya Kenya

"Kama unaharibu mazingira basi ni lazima ulipe kwa kusaidia kuweka mazingira safi", anasema John Mbadi waziri wa fedha.

Serikali ya Kenya inapanga kukusanya kiasi cha dola bilioni 1.2 kwa kurejesha baadhi ya kodi ambazo hazikupendwa zilizokuwemo katika mswada wa fedha ambao ulifutwa wakati wa maandamano ya mitaani, waziri wa serikali alisema.

Rais William Ruto alionya juu ya upungufu wa fedha baada ya kuamua mwezi Juni kutupilia mbali ongezeko la kodi lililozua utata, baada ya siku ya umwagaji damu jijini Nairobi iliyoshuhudia bunge kuvamiwa na polisi walifyatua risasi za moto kwa waandamanaji.

Waziri wa Fedha John Mbadi alikiambia kituo cha binafsi cha Citizen TV siku ya Jumapili kwamba serikali ilifikiria kuhusu hatua 49 za kodi ili kujaribu kukusanya takriban dola bilioni 1.2.

Polisi Kenya wakati walipokabiliana na maandamano nchini humo maarufu Gen-Z
Polisi Kenya wakati walipokabiliana na maandamano nchini humo maarufu Gen-Z

Hatua hizi ni pamoja na kurejeshwa kwa “kodi ya mazingira” kwenye bidhaa kama vile vifaa vya elektroniki pamoja na vile vilivyofungwa kwenye mifuko ya plastiki, ambayo serikali inasema inalenga kupunguza taka. "Kama unaharibu mazingira basi ni lazima ulipe kwa kusaidia kuweka mazingira safi", Mbadi alisema.

Mbadi ni mmoja wa vigogo wanne wa upinzani waliojiunga na baraza la mawaziri lililobadilishwa baada ya Ruto kuapa kuunda serikali thabiti ili kujaribu kushughulikia wasiwasi wa waandamanaji, wakiongozwa kwa kiasi kikubwa na vijana nchini Kenya maarufu Gen-Z.

Forum

XS
SM
MD
LG