Muungano huo unaojumuisha vyama vya siasa, vyama vya wafanyakazi na mashirika ya kiaraia, uliongoza maandamano dhidi ya rais wa zamani Alpha Conde kabla ya kuondolewa kwake madarakani katika mapinduzi ya kijeshi mwaka jana.
Mvutano umekuwa ukiongezeka kwa miezi kadhaa kati ya FNDC na utawala wa kijeshi, na kuibua katika taarifa ya muungano huo siku ya Jumatatu ukisema kwamba utafanya maandamano Agosti 17.
Amri hiyo ya Jumamosi, iliyosainiwa na waziri wa utawala wa ndani Mory Conde ikitangaza kuvunjwa kwa FNDC, imethibitishwa na AFP Jumanne.
“Kundi hilo lililojiteua linaloitwa FNDC, limevunjwa kuanzia tarehe ya kutiwa saini amri hii,” uamuzi huo umesema.
Amri hiyo imesema” FNDC kwa kuendesha harakati zake inajihusisha na mashambulizi mabaya yanayofanywa wakati wa maandamano yaliyopigwa marufuku, mashambulizi dhidi ya watu wasiokubaliana na itikadi yao, na mashambulizi yanayolenga maafisa wa usalama.”