Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:28

Serikali ya Gambia kumfungulia mashtaka rais wa zamani Yahya Jammeh


Rais wa zamani Yahya Jammeh, wakati wa kuhitimisha kampeni ya uchaguzi ya chama chake cha APRC, mjini Banjul, November 29, 2016. Picha ya AFP
Rais wa zamani Yahya Jammeh, wakati wa kuhitimisha kampeni ya uchaguzi ya chama chake cha APRC, mjini Banjul, November 29, 2016. Picha ya AFP

Serikali ya Gambia Jumatano imesema itamfungulia mashtaka rais wa zamani Yahya Jammeh kwa mauaji, ubakaji, mateso na madai ya uhalifu mwingine uliofanywa chini ya utawala wake wa zaidi ya miaka 20.

Wizara ya sheria imesema imekubali mapendekezo yote isipokuwa mawili kati ya 265 yaliyotolewa na tume ambayo ilichunguza madai ya uhalifu uliofanywa na serikali chini ya kiongozi huyo wa zamani kuanzia Julai 1994 hadi Januari 2017.

Jammeh anaishi uhamishoni nchini Guinea Equatorial, ambayo haina mkataba na Gambia wa kumrejesha nchini mwake.

Serikali imesema itawafungulia mashtaka washukiwa wote 77 waliotajwa katika ripoti ya tume ya ukweli, maridhiano na fidia iliyocheleweshwa mara mbili, akiwemo makamu rais wa zamani Isatou Njie-Saidy.

“Kwa miaka 22, Yahya Jammeh aliitawala Gambia kimabavu,” serikali imeandika katika waraka.

“Wakati wa utawala wake, mauaji ya kiholela, ubakaji, mateso , watu kutoweka, na vitendo vingi vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ilikuwa sehemu ya maovu yaliyotendwa na jeshi lake.”

XS
SM
MD
LG