Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 10:00

Serikali ya Chad yawaachilia huru waasi 380 baada ya kuwaondolea kifungo cha maisha jela


Rais wa Chad Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno
Rais wa Chad Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno

Serikali ya Chad imesema iliwaachilia huru waasi 380 Jana Jumatano baada ya kuwaondolea kifungo cha maisha jela walichohukumiwa kufuatia kifo cha rais wa zamani Idriss Deby Itno.

Katika hafla iliyopeperushwa kwenye televisheni, mwandishi wa habari wa AFP akiwa kwenye jela la Klessoum karibu na mji mkuu N’Djamena aliwaona wanaume 30 wamevaa sare za wafungwa zenye rangi nyeusi na nyeupe wakisimama mbele ya maafisa wa serikali ambao waliwapa cheti chao cha kuachiliwa.

Wafungwa wengine 350 waliachiliwa huru katika hafla iliyofanyika kabla, alisema waziri wa sheria Mahamat Ahmat Alhabo, ambaye alihudhuria hafla hiyo.

Tarehe 21 Machi, zaidi ya waasi 400 walihukumiwa na mahakama ndani ya jela kufuatia kesi ya watu wengi.

Walisamehewa siku nne baadaye na kiongozi wa utawala wa kijeshi na rais wa mpito Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno.

Waasi hao ni wanachama wa the Front for Change and Concord in Chad ( FACT), kundi kubwa la upinzani lenye silaha nchini humo.

Walikamatwa baada ya kundi lao la FACT kufanya shambulizi kaskazini mwa Chad kutokea katika ngome zake nchini Libya mapema mwaka 2021.

Shambulizi hilo lilisababisha kifo cha Idriss Deby Itno, baba wa rais wa sasa, ambaye aliitawala Chad kimabavu kwa miongo mitatu iliyopita, ambaye alikuwa eneo hilo kuongoza wanajeshi katika mapigano na waasi.

XS
SM
MD
LG