Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 23:05

Serikali ya Afrika kusini ipo njia panda kuhusu ICC, Putin akitarajiwa kuzuru nchini humo


Rais wa Russia Vladimir Putin ambaye mahakama ya ICC inataka akamatwe kwa uhalifu wa vita nchini Ukraine
Rais wa Russia Vladimir Putin ambaye mahakama ya ICC inataka akamatwe kwa uhalifu wa vita nchini Ukraine

Serikali ya Afrika kusini inafikiria la kufanya endapo rais wa Russia Vladimir Putin atakubali mwaliko wa kuhudhuria kongamano la kiuchumi nchini humo.

Mwaliko huo ulikuwa umetolewa awali kabla ya mahakama ya uhalifu ya kimataifa ICC kutoka hati ya kutaka Putin akamatwe.

Mahakama ya ICC, mjini Hague ilitoa hati mwezi March, ya kutaka rais wa Russia Vladimir Putin akamatwe kuhusiana na uhalifu wa kivita kutokana na kuwahamisha Watoto kutoka Ukraine hadi Russia.

Afrika kusini imetia saini mkataba wa kuundwa kwa ICC ambao unazitaka nchi wanachama kutekeleza amri zake.

Lakini Afrika kusini ni mshirika mkubwa wa Russia, na imejizuia kukosoa uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Afrika kusini ilifanya mazungumzo na waziri mkuu wa Russia Sergey Lavrov mapema mwaka hu una kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi na wanajeshi wa Russia mwezi Februari, yaliyofanyika Afrika kusini.

Waziri wa mambo ya nje wa Afrika kusini Naledi Pandor, ameiambia radio moja ya Afrika kusini kwmaba serikali ilikuwa inasubiri ushauri wa kisheria kutoka kwa maafisa wake, kabla ya kuamua cha kufanya.

"Ni hali ngumu lakini unajua baraza la mawaziri linahitaji kujadili swala hili. Nitakapokuwa na ushauri wa kutosha, nitaliwasilisha kwa baraza la mawaziri. Uamuzi wetu utazingitia maoni ya serikali kwa jumla."

Hata hivyo, waziri huyo hakusema iwapo kuna uwezekano wa kufuta mwaliko aliopewa rais Putin kuhudhuria kongamano la kiuchumi la nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika kusini, maarufu BRICS.

Kongamano hilo litafanyika mwezi August. Moscow haijasema iwapo Putin atahudhuria.

Waziri Pandor pia ameikosoa mahakama ya ICC kwa kile amekitaja kama msimamo tofauti dhidi ya viongozi wanaoshutumiwa kwa uvunjaji wa sheria ya kimataifa. Amedai kwamba ICC inayalenga baadhi ya mataifa.

Lakini waziri wa upinzani anayehusika na maswala ya uhusiano wa kimataifa Darren Bergman, kutoka chama cha upinzani cha Democratic Allliance, amesema kwamba ni lazima serikali ya Afrika kusini iheshimu mkataba wa ICC.

"Chama cha Democratic alliance kinaamini kwamba baraza la mawaziri halistahili kumwalika rais Putin na kwa hivyo, linastahili kufuta mwaliko huo. Kama hawatafanya hivyo, wawe tayari kumkamata Putin."

Mchambuzi wa siasa za Russia, Steven Gruzd, wa taasisi ya maswala ya kimataifa nchini Afrika kusini, ameiambia VOA kwamba kuna hatua tofauti serikali ya Afrika kusini inaweza kuchukua.

Mojawapo ni kufanya mkutano huo kwa njia ya mtandao, au kuondoa mwaliko wa Putin, au itafute njia ya kisheria ya kuhakikisha kwamba Putin hakamatwi kwa kuzingatia kwamba ni rais wa nchi.

"Tumeona hali kama hii. Mnamo mwaka 2015, aliyekuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir alikuja Afrika kusini kwa mkutano wa Umoja wa Afrika, na mahakama ya Afrika kusini iliamuru kwamba akamatwe. Amri hiyo hata hivyo haikutekelezwa na alikubaliwa kuondoka kupitia uwanja wa ndege wa kijeshi."

Msemaji wa idara ya uhusiano wa kimataifa ya Afrika kusini Lunga Ngqengelele, amesema kwamba huenda baraza la mawaziri likajadili swala hilo wiki hii.

XS
SM
MD
LG