Baraza hilo lenye mawaziri 24 ambalo limeundwa baada ya chama cha watu huru cha Akhannouch RNI kuwashinda waislamu walio madarakani katika uchaguzi mwezi uliopita, lina wanawake saba, wakati utawala uliopta ulikuwa na mawaziri wanawake wanne.
Serikali hiyo inaundwa kwa kiasi kikubwa na watu wenye taaluma wasioegemea vyama vya siasa, pamoja na mwanadiplomasia mkongwe Nasser Bourita ambaye ameshikilia nafasi yake kama waziri wa mambo ya nje, katika hali ya mivutano ya kikanda, haswa na nchi jirani ya Algeria.