Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 23:04

Serekali ya Chad na makundi ya uasi yatia saini makubaliano ya amani


Serekali ya kijeshi ya Chad, na baadhi ya makundi ya waasi wanaopigana katika nchi hiyo wametia saini ahadi zao nchini Qatar kabla ya mazungumzo ya kitaifa ya maridhiano yatakayofanyika baadaye mwezi huu.

Hata hivyo, kundi kubwa la uasi halikukubaliana na yaliyopo katika ahadi walizo afikiana.

Mkataba wa Jumatatu mjini Doha umeyataka makundi yote yaliyotia saini kusimamisha mapigano kabla ya mazungumzo yaliyopangwa kufanyika Agosti 20 katika mji mkuu wa Chad, N’Djamena.

Serekali ya kijeshi ya Chad imekubali kutochukua hatua zozote za kipolisi ama kijeshi dhidi ya makundi yaliyotia saini katika mataifa ya jirani.

Hata hivyo kundi kuu la uasi la FCCC halikutia saini hati ya ahadi zao.

XS
SM
MD
LG