Sera hiyo ambayo ilitangazwa mwezi Aprili, itairuhusu Uingereza kupeleka maelfu ya wahamiaji huko Rwanda ambao huwasili kwenye mwambao wake kutoka zaidi ya kilomita 6,400.
Akitangaza uamuzi wa mahakama hiyo, jaji Clive Lewis amesema ni halali kwa Uingereza kufanya mipango na serikali ya Rwanda kuwapeleka waomba hifadhi nchini humo na maombi yao ya kupewa hifadhi yataamuliwa huko.
Amesema “Katika mazingira hayo, kuhamishwa kwa waomba hifadhi nchini Rwanda kunaheshimu mkataba wa wakimbizi na majukumu mengine ya kisheria kwa serikali, likiwemo jukumu lililowekwa na sheria ya haki za binadamu ya mwaka 1998.”
Lakini jaji huyo amesema, waziri wa mambo ya ndani, waziri wa usalama lazima wazingatie ipasavyo mazingira “ya maombi ya kila mtu binafsi.”