Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 05:04

Baraza la Seneti lashindwa kufuta huduma ya Obamacare


Seneta John McCain
Seneta John McCain

Baraza la Seneti la Marekani mapema Ijumaa limeshindwa kufuta baadhi ya vipengele vya sheria ya huduma nafuu ya afya.

Sheria hiyo ya afya ambayo imedumu kwa miaka saba, ni maarufu kama Obamacare.

Wabunge wa chama cha Republikan, Seneta John McCain wa Arizona, Lisa Murkowsi wa Alaska na Susan Collins wa Maine walichukuwa msimamo mmoja katika kadhia hiyo.

Wote watatu walipiga kura kuungana na Wademocrat kwa kupata kura 49 dhidi ya 51 ili kuzuia juhudi za Warepublican kuifuta sheria hiyo.

Rais wa marekani Donald Trump aliandika kwenye mtandao wake wa Twitter muda mfupi baada ya kura kuwabeza warepublican ambao waliungana na wademocrat. “

Warepublican watatu na wademocrat 48 wamewaangusha watu wa marekani.

“Kama nilivyosema kutoka mwanzo wacha OBAMACARE ianguke,” Rais aliandika.

XS
SM
MD
LG