Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 12:36

Seneta Collins athibitisha kumuunga mkono Jaji Brown


Jaji mteule wa mahakama ya juu Marekani Ketanji Brown Jackson lipokutana na seneta wa Maine Susan Collins mjini Washingon
Jaji mteule wa mahakama ya juu Marekani Ketanji Brown Jackson lipokutana na seneta wa Maine Susan Collins mjini Washingon

Seneta wa Maine Susan Collins alisema  Jumatano kuwa  atapiga kura kumthibitisha Jaji Ketanji Brown Jackson, akiwapa Wademokrat  walau kura moja ya warepublican na akiwahakikishia kuwa Jackson atakuwa mwanamke wa kwanza Mweusi katika Mahakama ya Juu.

Collins alisema katika taarifa yake kwamba alikutana na Jackson mara ya pili baada ya siku nne za kusikilizwa kwake wiki iliyopita na kuamua kuwa ana uzoefu, sifa na uadilifu wa kuhudumu kama Jaji mmojawapo katika Mahakama ya Juu.

Kwa hivyo, nitapiga kura kumthibitisha katika nafasi hii, Collins alisema.

Uungasji mkono wake unawapa Wademokrat walau kura moja katika baraza la Seneti lililogawiki sawa kati ya wademokrat na warepublikan 50-50 na kuna uwezekano kuwaokoa dhidi ya kutumia kura ya kuvunja usawa ya Makamu Rais Kamala Harris kuthibitisha chaguo la Rais Joe Biden. Inatarajiwa kwamba Wanademokrasia wote 50 watamuunga mkono Jackson, ingawa Mdemokrat mmoja mashuhuri mwenye msimamo wa wastani, Seneta wa Arizona Kyrsten Sinema, bado hajasema jinsi atakavyopiga kura yake.

Jackson, ambaye atachukua nafasi ya Jaji anayestaafu Stephen Breyer, atakuwa jaji wa tatu Mweusi, baada ya Thurgood Marshall na Clarence Thomas, na mwanamke wa sita. Pia atakuwa wakili wa utetezi wa kwanza wa umma wa zamani katika mahakama hiyo.

XS
SM
MD
LG