Katika siku mbili zilizopita, mtu mmoja ameuawa katika mapigano kati ya polisi wa kutuliza ghasia na wafuasi wa Ousmane Sonko, ambaye anasema kuwekwa kwake kizuizini siku ya Jumatano kufuatia madai ya ubakaji kuna ushawishi wa kisiasa.
NetBlocks ilisema programu za mitandao ya kijamii na ujumbe ikiwa ni pamoja na Facebook, WhatsApp, na Youtube yamewekewa masharti mapema Ijumaa kabla ya maandamano yaliyo pangwa kufanywa na asasi za kiraia na vyama vya upinzani yakiongozwa na harakati ya maandamano iitwayo Y'en a Marre.
Sonko, mkaguzi wa kodi mwenye umri wa miaka 46 ambaye alishika nafasi ya tatu akiwa na asilimia 15 ya kura katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2019, anapata uungaji mkono mkubwa miongoni mwa vijana wa Senegal. Anakabiliwa na uchunguzi baada ya kuvuliwa kinga yake ya ubunge wiki iliyopita.