Mshindi wa Kiatu cha Dhahabu Aymen Mahious wa Algeria alipata fursa ya kushinda kiatu hicho kwa wanasoka wanaocheza katika nchi waliko zaliwa alipokwenda kupiga mkwaju wa penati wa 10.
Lakini jaribio lake lilikuwa dhaifu na lilienda moja kwa moja kwa kipa Pape Sy, ambaye aliokoa kirahisi, na kuziacha timu zikiwa zimefungana mabao 4-4, na kulazimika kuongezwa upigaji wa mikwaju hiyo na kupatikana mshindi.
Ousmane Diouf aliweka ndani penati yake kwa utulivu na kuiongoza Senegal mbele huku kukiwa na kelele kutoka kwa watu wengi katika umati wa watu 39,120 ambao walikuwa katika Uwanja wa Stade Nelson Mandela mjini Algiers.
Ahmed Kendouci ilibidi afunge ili kuweka hai matumaini ya Waalgeria kupata ushindi, lakini shuti lake lilipaa juu ya lango na Senegal wakautwaa ubingwa.
Timu hiyo yenye maskani yake nchini Senegal ilishinda mwaka mmoja tu baada ya timu kamili ya Senegal, wakiwemo nyota kama Sadio Mane, kuifunga Misri kwa mikwaju ya penalti na kushinda kombe lao la kwanza la soka la Mataifa ya Afrika.
Facebook Forum