Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:27

Senegal yakata tiketi ya kwanza kuingia kwa timu za Afrika kuingia raundi ya pili


Kocha wa timu ya Senegal Aliou Cisse aliokuwa akizungumza huko Spartak Stadium, Moscow, Russia - June 19, 2018.
Kocha wa timu ya Senegal Aliou Cisse aliokuwa akizungumza huko Spartak Stadium, Moscow, Russia - June 19, 2018.

Timu ya taifa ya Senegal Simba wa Teranga imekuwa timu ya kwanza ya Afrika kufanikiwa kuingia raundi ya 16 katika michuano ya mwaka huu baada ya kuifunga Ecuador bao 2-1.

Senegal iliingia kwenye michuano kwa kusua sua ikimkosa mchezaji wake hatari Sadio Mane lakini ikajirekebisha baada aya kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Uholanzi.

Itakumbukwa wakiwa wamefungana pointi nne na Japan katika Kundi H, Senegal ilitupwa nje ya Kombe la Dunia la 2018 kwa sababu ya kupokea kadi nyingi za njano.

Mabao ya Senegal yalifungwa na Ismaila Sar kunako dakika ya 44 kwa njia ya penati na Ecuador walisawazisha katika dakika ya 66 kupitia kwaMoises Caicedo lakini halikudumu kwani katika dakika ya 70 Kalidou Koulibaly aliipatia timu yake bao la ushindi.

Marekani yavuka

Nayo timu ya Marekani imeweka rekodi ya kuingia raundi ya pili ya kombe la dunia baada ya kuishinda Iran katika mchezo mkali na wa kusisimua ambao uliofanyika katika uwanja wa Al- Thumama.

Marekani ilishindwa kufanya hivyo kwa kutolewa mapema katika fainali za mwaka 2018.

Winga anayechezea timu ya Chelsea Christian Pulisic alifanikiwa kufunga bao pekee katika dakika ya 38 baada ya kuunganisha pasi na kuweka mpira wavuni na hatimaye aligongana na kipa wa Iran na kulala chini kwa dakika kadhaa akitibiwa baada ya kufunga bao hilo na alishindwa kurejea uwanjani kuendelea katika kipindi cha pili.

Ushindani mbaya wa kisiasa kati ya Marekani na Iran ulitawala kipindi cha kuelekea mchuano huo wa Kombe la Dunia Jumanne.

Rais Biden afurahia ushindi wa Marekani

Na wakati huo huo baada ya kumaliza hotuba yake siku ya Jumanne alasiri katika Jiji la Bay, Michigan, Rais wa Marekani Joe Biden alipeana mikono na wananchi kisha akarudi kwenye jukwaa na tangazo lisilotarajiwa: akisema “ Marekani 1 - Iran bila. Mchezo umekwisha.”

Umati wa wafanyakazi katika kiwanda cha utengenezaji wa SK Siltron CSS ulianza kuimba, “U.S.A.U.S.A!”

Kisha akatoka kwenye jukwaa na kurudi kusalimia wananchi akionekana kufurahia ushindi huo.

Marekani sasa watapambana na Uholanzi katika raundi ya pili siku ya Jumamosi.

Uingereza yaingia raundi ya pili

Nayo timu ya Uingereza imefanikiwa kuingia raundi ya pili baada ya kuichapa Wales mabao 3-0 katika uwanja wa Ahmad Bin Ali na kuongoza kundi B siku ya jumanne .

Kipindi cha kwanza kilitawaliwa na Uingereza lakini hawakuweza kupata bao hadi kwenda mapumziko wakiwa sare.

Kipindi cha pili waliingia na nguvu kubwa na kujipatia mabao yote matatu ambayo yalifungwa na Marcus Rushford kunako dakika ya 50 na Phil Foden aliongeza bao la pili katika dakika ya 51 na Rushford tena akamalizia bao la tatu katika dakika ya 68.

Nao wenyeji Qatar ambao tayari walikuwa wamekwishatolewa kwenye michuano hiyo walifungwa bao 2-0 na Uholanzi .

Mabao ya Uholanzi yalifungwa na Cody Gakpo na Frenkie de Jong katika dakika za 26 na 49 na kwa maana hiyo sasa Uholanzi itakwaana na Marekani katika raundi ya pili.

Kocha wa timu ya Qatar Sanchez anasema uzoefu ndio umeiponza timu yake ikiwa ni kwa mara ya kwanza wamepoteza mechi 3 mfululizo .

Lakini anasema kuwa amefurahishwa kuwa sehemu ya kombe kubwa kabisa duniani na kushiriki kwa timu yake.

XS
SM
MD
LG