Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 18:45

Senegal yaanza ujenzi wa kiwanda cha kuondoa chumvi kwenye maji

Rais wa SeneGAL Macky Sall akihutubia mkutano mjini Brussells.
Rais wa SeneGAL Macky Sall akihutubia mkutano mjini Brussells.

Senegal imeanza kazi ya kujenga kiwanda cha kwanza cha kuondoa chumvi katika maji nchini humo, mpango unaopingwa na wakosoaji ambao wanadai  ni wa gharama kubwa na hatari kwa mazingira.

Senegal imeanza kazi ya kujenga kiwanda cha kwanza cha kuondoa chumvi katika maji nchini humo, mpango unaopingwa na wakosoaji ambao wanadai ni wa gharama kubwa na hatari kwa mazingira.

Rais Macky Sall siku ya Jumanne alizindua kwa sherehe kazi ya kujenga kiwanda katika wilaya ya Mamelles mjini Dakar yenye lengo la kupunguza uhaba wa maji katika mji mkuu huo.

Sall alisema mradi huo wenye utata na ambao haujawahi kushuhudiwa" ulikuwa hatua muhimu katika mpango wa miundo mbinu iliyoanzishwa ili kuifikisha Senegal katika hali ya uchumi unaoibukia ifikapo 2035.

Kituo hicho cha pwani kitaondoa chumvi kwenye maji kutoka Atlantiki, na kilele cha ujazo wa mita za ujazo 100,000 (zaidi ya galoni milioni 25) kwa siku.

Mradi pia unahusu ukarabati wa zaidi ya kilomita 300 za mabomba ya maji.

XS
SM
MD
LG