Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 08, 2025 Local time: 18:47

Senegal: Wafuasi wa Sonko wakabiliana na polisi


Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko akilakiwa na wafuasi wake mjini Dakar Feb 16, 2023
Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko akilakiwa na wafuasi wake mjini Dakar Feb 16, 2023

Makabiliano yalizuka Ijumaa usiku kati ya polisi na wafuasi wa kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, wakato msafara wake wa magari ulipowasili mjini Kolda, kusini mwa nchi hiyo.

Sonko alikuwa akisafiri kuelekea mji mkuu wa Dakar, ambako anatarajiwa kufika mahakamani wiki ijayo kujibu mashtaka ya ubakaji na kutoa vitisho vya mauaji.

Amekanusha mashtaka dhidi yake na huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani endapo atapatikana na hatia.

Sonko hivi karibuni alikuhumiwa kifungo cha miezi sita bila ya kuzuiliwa gerezani, na alitangaza kwamba hataendelea kuheshimu amri za kutakiwa kufika mahakamani.

Wafuasi wake wameitisha maandamano kupinga kesi dhidi ya Sonko, wanazosema kwamba zina ushawishi wa kisiasa ili kumzuia asigombee urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao 2024.

Sonko alikuwa amebadilisha safari yake ya kilomita 500 kuwa msafara wa magari aliouita kuwa wa uhuru, akitoa wito kwa wafuasi wake kumfuata kutoka mji wa nyumbani kwake wa Ziguinchor, kusini mwa Senegal, hadi mji mkuu Dakar.

Serikali imeapa kwamba itakabiliana na tukio lolote litalotaka kuathiri utulivu na amani.

Forum

XS
SM
MD
LG