Niang alipelekwa hospitali Jumamosi jioni baada ya afya yake kuzorota kama matokeo ya mgomo wake wa njaa wa hivi karibuni, amesema Moussa Sarr, mmoja wa mawakili wake.
Katika kesi iliyozusha wasiwasi wa kimataifa, Niang alikamatwa tarehe 6 Novemba na kushtakiwa kwa kufichua habari zinazoweza kuhujumu ulinzi wa taifa.
Alianza mgomo wa kula tarehe 2 Disemba na alipelekwa baadaye kwenye hospitali baada ya afya yake kuzorota.
Aliachiliwa kwa muda lakini alikamatwa tena baadaye tarehe 20 Disemba, ambapo alianza mgomo mwingine wa kula.
Niang, mkurugenzi wa gazeti la mtandaoni Dakar matin, ana wafuasi wengi nchini Senegal kwa taarifa zake za mara kwa mara kuhusu habari zinazojiri nchini.