Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:34

Senegal yaakhirisha kumrejesha Habre nchini Chad


Rais wa zamani wa Chad, Hissene Habre mwenye miwani akiwa Dakar nchini Senegal, mwaka 2005
Rais wa zamani wa Chad, Hissene Habre mwenye miwani akiwa Dakar nchini Senegal, mwaka 2005

Serikali ya Senegal imeamua kutomrejesha Rais wa zamani wa Chad, Hissene Habre, nchini kwake kwa kuhofia usalama wake

Waziri wa mambo ya nje wa Senegal anasema serikali yake imeamua kutomrejesha Rais wa zamani wa Chad, Hissene Habre, saa kadhaa kabla kupelekwa nyumbani Jumatatu.

Madicke Niang amesema Senegal iliamua kuakhirisha kutomkabidhi kufuatia ombi la kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na masuala ya haki za binadamu, Navi Pillay.

Katika taarifa iliyotolewa mapema Jumapili, bibi, Pillay amesema kwamba Senegal kama nchi iliyotia saini mkataba dhidi ya mateso, haiwezi kumkabidhi mtu yeyote kwenda kwenye nchi ambayo kuna khofu zinazoaminika atakuwa hatarini kwa kufanyiwa manyanyaso.

Bwana Habre ambaye aliondolewa madarakani kwa njia ya mapinduzi mwaka 1990 na Rais wa sasa wa Chad, Idriss Deby alihukumiwa adhabu ya kifo bila kuwepo kwa kuwatesa na kuwauwa wapinzani wa kisiasa. Amekuwa akiishi Senegal tangu mapinduzi yalipotokea.

Makundi kadhaa ya haki za binadamu pia yameelezea wasi wasi kuhusu nia ya Senegal kumpeleka bwana Habre nyumbani. Alioune Tine, ambaye ni rais wa taasisi za haki za binadamu Afrika, alisema huwezi kumpeleka mtu kwenda kwenye nchi ambayo inafanya unyanyasaji na inakubaliana na adhabu ya kifo.



XS
SM
MD
LG