Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 20:10

Senate ya Marekani yaidhinisha Sweden na Poland kujiunga na NATO


Kiongozi wa waliowengi kwenye bunge la Senate , Marekani Chuck Schumer
Kiongozi wa waliowengi kwenye bunge la Senate , Marekani Chuck Schumer

Bunge la Senate la Marekani Jumatano limepiga kura ya 95-1 ya kuruhusu Sweden na Finland kujiunga na NATO, ikionekana kuwa hatua kubwa kwenye shinikizo la mataifa ya magharibi dhidi ya Russia.

Kiongozi wa walio wengi katika bunge hilo Chuck Schumer amesema kwamba kura hiyo ni muhimu sana kwa usalama wa Marekani na kote ulimwenguni, na kwamba uwepo wa Sweden na Finland utaimarisha NATO hata zaidi, hasa wakati huu ambapo Putin amefanya mashambulizi yasio na maana dhidi ya Ukraine.

Amesema kwamba kwa kufanya hivyo, Putin anaimarisha uwezo wa NATO. Kabla ya upigaji kura huo, mwenyekiti wa kamati ya uhusiano wa kimataifa kwenye bunge hilo Bob Manendez alisema kwamba ungetuma ujumbe mkali kwa Russia kutokana na uvamizi wake wa Ukraine. Hata hivyo mrepablikan Josh Hawley ambaye ndiye pekee aliyepinga kura hiyo amesema kwamba inaenda kinyume na sera za kigeni za Marekani.

XS
SM
MD
LG