Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 10, 2024 Local time: 20:28

Maseneta Marekani wakubaliana kufungua tena shughuli za Serikali Kuu


Wafanyakazi katika bunge la Marekani wakisubiri kuingia ofisini katika siku ya tatu ya kufungwa kwa serikali kuu, Jan. 22, 2018.
Wafanyakazi katika bunge la Marekani wakisubiri kuingia ofisini katika siku ya tatu ya kufungwa kwa serikali kuu, Jan. 22, 2018.

Baraza la Senate la Marekani Jumatatu limefikia makubaliano ya kupitisha kwa mpango wa matumizi na kuifungua tena serikali kuu baada ya kufungwa kwa baadhi ya shughuli za serikali kwa siku tatu.

Wademocrat 33 walijiunga na warepublican 48 kumaliza mjadala katika baraza la senate lenye wanachama 100 kuongeza muda kwa mswaada wa matumizi ya serikali kuu mpaka Februari 8. Hatua hiyo ya haraka ilitarajiwa kwenda kwenye baraza la wawakilishi, baada ya hapo mswaada utakwenda White House kwa rais Donald Trump ili kuutia saini.

“Leo ni siku ya kushereheka,” mrepublican, Seneta Susan Collins wa Maine amesema. “Serikali inapofungwa, inabainisha kushindwa kutawala.”

Awali kiongozi wa walio wetu katika baraza la senate, Mitch McConnell wa Kentucky amewahakikishi wademocrat katika senate kuwa watazungumzia masuala mbali ya uhamiaji, ikiwemo maelfu ya wahamiaji ambao hawana makaratasi halali, ambao waliingizwa Marekani kama watoto ambao hali yao ya baadaye ndiyo ni suala kuu linalojadiliwa baada ya Trump kuamua kufuta program ambayo inawaruhusu kufanya na kusoma nchini Marekani.

Kupitisha mageuzi ya uhamiaji kunahitaji siyo baraza la senate peke yake. Hatua katika baraza la wawakilishi na sahihi ya Trump pia vinahitajika kupitisha mageuzi hayo.

White House imepeleka ishara mchanganyiko kwa kile ambacho rais atakikubali kama makubaliano ya mwisho ya uhamiaji. Warepublican katika bunge, wakati huo huo, wamesema si lazima wakubaliane na ahadi ambazo zimetolewa kwenye baraza la senate.

“Wanachofanya kwenye senate ni juu yao,” amesema mbunge wa Oklahoma, Tom Cole.

XS
SM
MD
LG