Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 18:47

Sejjusa atasimamishwa katika mahakama ya kijeshi Uganda


Jenerali David Sejusa, mkosoaji wa Rais Yoweri Museveni
Jenerali David Sejusa, mkosoaji wa Rais Yoweri Museveni

Aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi nchini Uganda Jenerali David Sejusa atafikishwa katika mahakama ya kijeshi Jumanne kujibu mashtaka yanayohusiana na kupanga njama za kuipindua serikali yake Rais Yoweri Museveni.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:54 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Jenerali Sejusa, mmoja wa makamanda wakuu katika jeshi la Uganda anadaiwa kutoa matamshi ya kuichafua serikali ya Rais Museveni kwa kumhusisha na wizi wa kura katika uchaguzi mkuu nchini Uganda na Kenya.

Jenerali huyo alikimbilia uhamishoni mwaka 2013 baada ya kudai kwamba kulikuwepo na mipango ya kuwauwa maafisa wakuu serikalini hasa wale wa idara ya usalama waliokuwa wakipinga mpango wa kutaka brigedia Muhozi kainerugaba, mwanae Rais Museveni kuwa Rais wa Uganda baada ya baba yake kuondoka madarakani.

XS
SM
MD
LG