Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 22:14

Mfalme Salman aahidi kuendeleza sera za Saudia


Mfalme mpya wa Saudi Arabia Salman
Mfalme mpya wa Saudi Arabia Salman

Mfalme mpya wa Saudi Arabi, Salman, anaahidi kuendeleza sera za kaka yake, hayati Mfalme Abdullah, ambaye alizikwa Ijumaa katika mji mkuu wa nchi hiyo Riyadh.

Abdullah ambaye alifariki Alhamisi usiku baada ya kuungua kwa muda mrefu, alizikwa katika kaburi la kawaida katika maziko yaliyohudhuriwa na viongozi wa kiarabu na kutoka nchi kadhaa za kiislamu. Akiwa mmoja wa wafalme wachache duniani waliotokea moja kwa moja katika damu ya kifalme, Abdullah inaaminika alikuwa na umri wa miaka 90 na hivi karibu alilazwa hospitali akiwa na matatizo ya mapafu.

Baada ya kufariki kwake Abdullah alisifiwa na kukosolewa na watu kadhaa. Wakati huo huo, katika nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta utawala wa Kisunni ulichukua hatua za haraka kuhakikisha kuna kipindi kizuri cha mpito.

Mfalme mpya, ambaye anadhaniwa kuwa na umri wa miaka 79, amekuwa mrithi wa ufalme na waziri wa ulinzi tangu 2012. Ndugu mwingine, Muqrin, aliteuliwa kuwa mrithi wa ufalme. Salman pia alimteuwa mpwa wake, Mohammed bin Nayef, kama naibu mrithi wa ufalme mpya na mtoto wake, Mohammed bin Salman, anakuwa waziri mpya wa ulinzi wa Saudi Arabia. Salman amesema atawaacha madarakani mawaziri wengi wa zamani.

XS
SM
MD
LG