Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 25, 2023 Local time: 17:00

Sarkozy ashindwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi


Mgombea kiti cha rais wa chama cha Socialist Francois Hollande akipongezwa na wafuasi wake baada ya kushinda duru ya kwanza.

Rais Nicolas Sarkozy anakua rais wa kwanza madarakani kushindwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi warais Ufaransa.

Mgombea kiti cha rais wa chama cha Socialist, Francois Hollande amepata ushindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa Ufaransa Jumapili, akijipatia asili mia 29.3 za kura. Mpinzani wake kiongozi wa vyama vya kihafidhina rais Nicplas Sarkozy amepata asili mia 26 za kura.

Wanasiasa hao wawili watapambana katika duru ya pili hapo Mai 6. Matokeo hayo yalitarajiwa kutokana na uchunguzi kadha wa maoni ulofanywa kabla ya uchaguzi wa Jumapili ukionesha kwamba Hollande atamshinda Sarkozy katika duru ya kwanza na ya pili..

Matokeo ambayo hayakutarajiwa ni kwa kiongozi wa kundi la mrengo wa kulia wenye siasa kali Bi. Marine le Pen kuchukua nafasi ya tatu, akifuatiwa na kiongozi wa siasa kali za mrengo wa kushoto Jean-Luc Melenchon.

Katika hotuba yake baada ya matokeo ya awali kutangazwa Bw Hollande alisema, ushindi wake unatokana na kushindwa kwa sera za rais wa kihafidhina wa Ufransa.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Salim Himidi mchambuzi wa masuala ya kisiasa mjini Paris anasema ushindi wa Hollande utaweza kurudisha tena hadhi ya Ufaransa duniani na kuwepo na uhusiano muzri zaidi na nchi za Kiafrika.

Katika hotuba yake rais Sarkozy amesema amepata ujumbe na anafahamu wasi wasi wa wananchi wa Ufaransa.

Kulikuwepo na wagombea kumi katika duru ya kwanza na Bw. Himidi anasema tisa kati ya hao walikua wanampinga Sarkozy.

XS
SM
MD
LG