Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 05, 2023 Local time: 17:17

Upinzani waelekea kwenye ushindi Sao Tome


Wapiga kura kwenye uchaguzi wa Sao Tome
Wapiga kura kwenye uchaguzi wa Sao Tome

Matokeo ya awali yanaonesha mpinzani ameshinda uchaguzi wa urais wa marudio nchini Sao Tome na Principe .

Matokeo ya awali yanaonesha mpinzani ameshinda uchaguzi wa urais wa marudio nchini Sao Tome na Principe baada ya Rais manuel Pinto da Costa kususia upigaji kura.

Tume ya uchaguzi katika taifa hilo lililopo Afrika magharibi ilisema kwenye mtandao wake Jumatatu kwamba waziri mkuu wa zamani Evaristo Carvalho alipata kiasi cha zaidi ya kura 42,000 katika koloni la zamani la Ureno, kutoka kwa wapigakura 111,000 waliojiandikisha.

Rais Pinto alijitoa kwenye uchaguzi huo akishutumu wizi wa kura na matatizo katika orodha ya wapiga kura katika barua yake kwa mahakama ya juu kisiwani humo.

XS
SM
MD
LG