Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 18:25

Mshukiwa wa shambulizi la Florida amefunguliwa kesi ya jinai


Abiria kwenye uwanja wa ndege wa Fort Lauderdale wakiwa katika hali ya taharuki. Januari 2, 2017.
Abiria kwenye uwanja wa ndege wa Fort Lauderdale wakiwa katika hali ya taharuki. Januari 2, 2017.

Mshukiwa wa shambulio la risasi kwenye uwanja wa ndege wa Florida amefunguliwa kesi Jumamosi kwa kosa la kuvuruga amani uliopelekea vifo, kwa mujibu wa taarifa za ofisi ya mwanasheria wa Miami, Marekani.

Esteban Santiago, 26, aliyewahi kutumikia jeshi la Marekani nchini Iraq anatuhumiwa kuua watu 5 na kujeruhi sita wengine katika shambulizi la risasi siku ya Ijumaa kwenue uwanja wa ndege wa kimataifa wa Fort Lauderdale na kusababisha hali ya hatari wakati maelfu ya watu waliokuwa na taharuki wakikimbia kujihami.

Iwapo atakutwa na hatia, Santiago anaweza kukabiliwa na adhabi ya kifo au hata kifungo cha maisha.

Santiago pia ameshtakiwa kwa makosa mengine mawili ya kutumia silaha kinyme cha sheria, wamesema maafisa katika ofisi ya mwendesha mashtaka.

Anashikiliwa bila ya kupewa dhamana na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa mara kwanza Jumatatu huko Florida.

Safari yake kwenda Florida

Mapema Jumaoisi, maafisa hao walisema katika mkutano na waandishi wahabari kwamba mshukiwa alisafiri " kwa kudhamiria" kwenda Fort Lauderdale kutekeleza azma yake, lakini sababu za kufanya hivyo bado hazijbainika.

Polisi walimhoji Santiago kwa saa kadhaa. Polisi wamesema amekuwa akitoa ushirikiano kwa wanaomhoji.

George Piro, ambaye ni mwakilishi maalum wa idara ya upelelezi ya FBI mwenye kuhusika na kitengo cha Miami amewaambia waandishi wa habari Jumamosi, "hatujaweza kufahamu sababu zilizopelekea shambulizi hili."

Polisi "wanaendelea kuangalia kwa kina iwapo kuna mahusiano yoyote ya kigaidi," kama ndiyo kishawishi, lakini ni "mapema mno katika uchunguzi huu" kutoa taarifa yeyote kuhusu dhamira ya shambulizi hili.

Uchunguzi wa afya ya akili

Huko Alaska, FBI na mkuu wa polisi wamesema Jumamosi kwamba Santiago aliwahi kufika katika ofisi zao mwezi Novemba.

Wamesema alikuwa katika hali ya hasira akitoa maelezo yasiyoeleweka na kusema alikuwa anasikia kelele zinazomwambia ajiunga na kundi la kigaidi la Islamic State.

Kama ilivyo kawaida mawakala wa FBI walimnyang'anya silaha yake.

Santiago alipelekwa kufanyiwa uchunguzi iwapo ana matatizo ya akili, lakini hakuoenkana na tatizo lolote.

Walimrudishia silaha yake mwezi Desemba. Mkuu wa polisi wa Anchorage, Christopher Tolley amesema haikuweza kujulikana mara moja iwapo ni silaha ile ile ilitumika katika shambulizi la Fort Lauderdale.

Piro ameeleza kuwa matatizo ya akili yanaweza kuwa yalipelekea kufanya shambulizi hilo. Baadhi ya ndugu wa Santiago waliwahi kusumbuliwa na matatizo ya akili.

Familia ya mshukiwa yazungumza

Mjomba wa Santiago, Hernan rivera, ameliambia gazetila Newark Star-Ledger, "kitu pekee ninachoweza kusema ni kuwa aliporejea kutoka Iraq alikuwa hajisikii vizuri."

Shangazi yake pia ameliambia gazeti hilo kuwa Santiago alilalwa hospitali baada ya kurejea kutoka Iraq. "Ilikuwa kana kwamba amechanganyikiwa," Ruiz Rivera alisema kwa lugha ya kispanish.

Kurudishiwa silaha

Kaka wa mshukiwa, Bryan Santiago amesema ndugu yake alikuwa na tatizo la kujizuia hasira tangu aliporeja kutoka Iraq. Aliongeza kuwa kitendo cha msimamizi wa FBI kumrudishia silaha ndugu yake ndiyo kilichomuingiza katika maangamizi haya.

Vyombo vya serikali huko Alask wametetea mazungumzo hayo na Esteban Santiago wakisema alikuwa hajavunja sheria wakati aliporipoti kwao "wakati akiwa amechanganyikiwa."

Katika mkutano na waandishi wa habari Jumamosi, Gavana Rick Scott amesema maafisa polisi walikuwa bado wanachambua vielelezo vya usahidi ili kufahamu kilichotokea.

Amesema ameongea na baadhi ya wale waliopigwa risasi ambao wamelazwa hospitali.

"Hiki ni kitendo cha kinyama. Familia moja niliyozungumza nayo walikuja hapa ili kustarehe kwa safari ya boti na mkewe akapigwa risasi," Scott amesema.

XS
SM
MD
LG