Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 08:14

Mshukiwa wa shambulizi la Florida kufikishwa mahakamani


Abiria katika uwanja wa ndege wa Fort Lauderdale wakiwa katika hali ya taharuki baada ya shambulizi.
Abiria katika uwanja wa ndege wa Fort Lauderdale wakiwa katika hali ya taharuki baada ya shambulizi.

Mshukiwa wa shambulizi la kinyama kwa kutumia silaha alilolifanya siku ya Ijumaa katika uwanja wa ndege wa Florida anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Jumatatu.
Esteban Santiago alifunguliwa mashtaka Jumamosi kwa kosa la kuvunja amani katika uwanja wa ndege wa kimataifa n akusababisha vifo. Ikiwa atakutwa na hatia, Santiago anakabiliwa na adhabu ya kifo au uwezekano wa kutumikia kifungo cha maisha kufuatia shambulio liliouwa watu watano.
Wakati polisi wanaendelea na uchunguzi kutafuta sababu zilizopelekea shambulizi hili, ndugu wa Santiago wamesema alikuwa amepatwa na msongo wa mawazo kufuatia miezi 11 ya kushiriki kwake katika vita vya Marekani nchini Iraq.
“Sio kila mtu anaweza kupata tatizo hili anaporejea kutoka vitani,” ndugu yake, Bryan Santiago amekiambia ktiuo cha televisheni cha CNN. “Baadhi wanakuwa vizuri, lakini wengine, wanachanganyikiwa.”

Kwa mujibu wa mama yao, Estebann Santiago, mwenye umri wa miaka 26, alikuwa ameathirika kwa kiwango kikubwa wakati alipoliona bomu likiripuka karibu na rafiki zake wawili alipokuwa anatumika nchini Iraq katika muda wote mwaka 2010 na 2011.

Ndugu mwingine wa mshukiw, Bryan Santiago amesema kaka yake aliomba msaada wa matibabu ya kisaikolojia lakini alipewa msaada kidogo mwisho wa mwaka jana baada ya kuingia katika ofisi za idara ya upelelezi - FBI huko Alaska.

FBI na mkuu wa polisi wamesema Jumamosi kwamba Santiago aliwahi kufika katika ofisi zao huko Anchorage Alaska mwezi Novemba akiwa amechanganyikiwa .

Wamesema alikuwa katika hali ya hasira akitoa maelezo yasiyoeleweka na kusema alikuwa anasikia kelele zinazomwambia ajiunge na kundi la kigaidi la Islamic State.

Kama ilivyo kawaida mawakala wa FBI walimnyang'anya silaha yake.

Santiago alifanyiwa uchunguzi iwapo ana matatizo ya akili, lakini hakuonekana na tatizo lolote.

Walimrudishia silaha yake mwezi Desemba. Mkuu wa polisi wa Anchorage, Christopher Tolley amesema haikuweza kujulikana mara moja iwapo ni silaha ile ile ilitumika katika shambulizi la Fort Lauderdale.

Piro ameeleza kuwa matatizo ya akili yanaweza kuwa yalipelekea kufanya shambulizi hilo. Baadhi ya ndugu wa Santiago waliwahi kusumbuliwa na matatizo ya akili.

XS
SM
MD
LG