Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 18, 2024 Local time: 10:10

Sanduku la ndege ya Egyptair lapatikana


Picha ya ndege ya shirika la egypair
Picha ya ndege ya shirika la egypair

Sanduku la pili la ndege lililokuwa na takwimu za ndege ya shirika la ndege la EgyptAir ambayo ilipata ajali katika bahari ya Mediterranean mwezi uliopita limepatikana, maafisa wa Misri wametangaza leo Ijumaa.

Sanduku la kwanza la takwimu kutoka ndege namba M804 ambayo ilikuwa ikielekea Cairo kutoka Paris lilionekana siku moja kabla.

Kupatikana kwa sanduku jingine ambalo lilihifadhi taarifa za namna ndege ilivyokuwa ikisafiri na muongozo mzima ulipatikana kutoka kwenye boti iliyokuwa ikitafuta mabaki ya ndege katika bahari ya Mediterrannean.

Kupatikana kwa mabaki ya ndege hiyo na sanduku la kunasa sauti kwenye usawa wa bahari kumeongeza matumaini kwamba maelezo juu ya ndege hiyo iliyopotea kiajabu na kusababisha vifo vya watu wote 66 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo huwenda yakapatikana.

XS
SM
MD
LG