Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 08:13

Sanders ampigia debe Clinton


Wademocrat wameanza mkutano wao mkuu Jumatatu huko Philadelphia wakitaka kuweka kando msimu wa uchaguzi wa awali wa kuwania uteuzi wa chama.

Baadhi ya sauti zenye nguvu zikizungumzia kuungana pamoja na mgombea wa urais Hillary Clinton.

Seneta wa Vermont, Bernie Sanders ambaye alishika nafasi ya pili katika kinyang’anyiro cha uteuzi wa chama cha Democrat, alisema nchi inahitaji uongozi ambao unawaleta watu pamoja badala ya kuwatusi walatino, waislam, wanawake, watu weusi na mashujaa wa vita.

Wakati Donald Trump yupo na harakati nyingi za kutusi kundi moja baada ya jingine, Hillary Clinton anafahamu kwamba mchanganyiko wetu ni moja ya nguvu zetu imara, alisema Sanders.

Alizungumzia kuhusu namna kampeni yake ilivyoweza kushinikiza chama cha Democrat kupitisha baadhi ya mapendekezo yake ikiwemo Wall Street, mageuzi katika fedha za kampeni na kupinga mikataba ya biashara kama Trans-Pacific Partnership.

Sanders alielezea kutoridhishwa kwake na namna utaratibu wa uteuzi ulivyokuwa, lakini alisema Clinton lazima awe rais ajaye wa marekani.

XS
SM
MD
LG