Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 15:48

Samuel Takyi aweka historia Ghana kwa kushinda medali baada ya miaka 29


Samuel Takyi wa Ghana akipambana na Ceiber Avila wa Colombia REUTERS / Yara Nardi
Samuel Takyi wa Ghana akipambana na Ceiber Avila wa Colombia REUTERS / Yara Nardi

Bondia Samuel Takyi wa Ghana alijihakikishia medali ya kwanza ya ndondi barani Afrika kwa kushinda katika pambano lake la robo fainali La uzani wa Feather

Bondia Samuel Takyi wa Ghana alijihakikishia medali ya kwanza ya ndondi barani Afrika kwenye michuano ya Olimpiki ya Tokyo kwa kushinda katika pambano lake la robo fainali ya uzani wa Feather dhidi ya Ceiber David Avila wa Columbia siku ya Jumapili. Takyi alishinda kwa wa pointi 3-2 baada ya raundi ya tatu kali na kuingia nusu fainali ambayo atakutana na Duke Ragan wa Marekani siku ya Jumanne.

Baada ya kufuzu kwa Takyi kwenye nusu fainali anajihakiki walau medali ya shaba, na kuwa raia wa Ghana wa nne tu kushinda medali ya ndondi katika historia ya Michezo ya Olimpiki.

Takyi ni mmoja wa mabondia wawili tu wa Kiafrika ambao bado wanashindana kwenye michuani ya Olimpiki ya Tokyo. Mwingine ambaye bado yupo katika michuano hiyo ni bondia wa kike wa Algeria katika uzani wa Light Imane Khelif ambaye atakuwa kwenye hatua ya robo fainali Jumanne dhidi ya Kellie Anne Harrington wa Ireland.

XS
SM
MD
LG