Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 19:50

Samantha Power asisitiza mzozo wa Ethiopia lazima uishe


Samantha Power, mkuu wa shirika la maendeleo ya kimataifa Marekani
Samantha Power, mkuu wa shirika la maendeleo ya kimataifa Marekani

Power siku ya Jumanne alikutana na wakimbizi nchini Sudan ambao wamekimbia Tigray, na alirejea msimamo wa Marekani, Umoja wa Mataifa, na wengine kwamba hatimaye kile kitakachowasaidia watu katika mkoa wa kaskazini mwa Ethiopia ni kumaliza vita ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa zaidi ya  miezi tisa

Mkuu wa shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani, Samantha Power anatarajiwa kukutana Jumatano na maafisa nchini Ethiopia wakati Marekani inaisihi serikali kuruhusu fursa ya wazi ya kufikisha misaada ya kibinadamu kwa mkoa wa Tigray.

Power, Jumanne alikutana na wakimbizi nchini Sudan ambao wamekimbia Tigray, na alirejea msimamo wa Marekani, Umoja wa Mataifa, na wengine kwamba hatimaye kile kitakachowasaidia watu katika mkoa wa kaskazini mwa Ethiopia ni kumaliza vita ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa zaidi ya miezi tisa.

Mji wa Mekele huko Tigray nchini Ethiopia. June 29, 2021.
Mji wa Mekele huko Tigray nchini Ethiopia. June 29, 2021.

Marekani imekuwa ikishinikiza pande zote huko Tigray kusitisha mapigano mara moja kwa matumaini kwamba watu waEthiopia ambao nimekutana nao hapa wataweza kurudi nyumbani, Power alisema katika maoni yake kwenye Twitter hapo Jumanne.

Mzozo huo umeleta mashambulizi mabaya dhidi ya raia unaathiri mamilioni na lazima uishe.

XS
SM
MD
LG