Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:28

Mshukiwa ugaidi wa Paris kushikiliwa Ubelgiji kwa wiki kadhaa


Mshukiwa mkuu kwenye mashambulizi ya ugaidi ya Ufaransa mwaka jana, Salah Abdeslam, atazuiliwa Ubelgiji kwa wiki kadhaa zijazo kabla ya kupelekwa Ufaransa.

Hayo yamesemwa mapema leo na wakili wa Abdesalam baada ya kusikilizwa hoja inayohusu kuzuiliwa kwake Ubelgiji. Wakili huyo amesema Abdesalam hawezi kupelekwa Ufaransa kabla ya kuhojiwa kuhusu kesi ya pili inayomkabili ya ufuataliaji risasi na polisi wakati wa kukamatwa kwake mjini Brussels mwezi uliopita.

Abdesalam alikamatwa Machi 18 baada ya kusakwa kwa zaidi ya miezi 4. Jumanne wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilimtaja Abdesalam kuwa gaidi wa kimataifa na kwa hivyo kutoa amri kwa watu wa Marekani kutoshirikiana naye kwa namna yoyote ile. Amri hiyo pia inazuilia mali yoyote anayoweza kuwa akimiliki hapa Marekani.

XS
SM
MD
LG