Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 21, 2025 Local time: 17:16

Sala kwa ajili ya Ebrahim Raisi imefanyika, maandalizi ya kuchagua rais mpya yameanza


waombolezaji waliojitokeza kumtolea heshima za mwisho rais Ebrahim Raisi, Tehran, May 22, 2024.
waombolezaji waliojitokeza kumtolea heshima za mwisho rais Ebrahim Raisi, Tehran, May 22, 2024.

Kiongozi wa juu kabisa wa Iran ameongoza sala kwa ajili rais wa nchi hiyo Ebrahim Raisi aliyefariki katika ajali ya helikopta, wakati utawala ukiharakisha maandalizi ya uchaguzi mkuu kumtafuta rais mpya.

Kuna wasiwasi kwamba uchaguzi huo huenda ukavuruga zaidi uhalali wa utawala huo huku imani kati ya raia wa Iran ikionekana kufifia.

Uchaguzi utafanyika Juni 28, kumchagua rais mpya baada ya kifo cha Ebrahim Raisi.

Uchaguzi huo utahitajika kuwaleta pamoja raia wa Iran ambao hawakuonyesha dhamira kubwa katika uchaguzi wa mwaka 2021 uliopelekea Raisi kuingia madarakani.

Idadi kubwa ya wapiga kura wamekuwa hawashiriki katika uchaguzi mkuu katika jamhuri hiyo ya kiislamu.

Kulingana na wachambuzi, raia wa Iran wana wasiwasi kuhusu uchumi wa taifa, na kubanwa kwa uhuru wa kujieleza.

Forum

XS
SM
MD
LG