Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 22:57

Sakata la Korosho : Mbunge atahadharisha kuzuka njaa Lindi, Mtwara


Mbunge Cecil Mwambe - Tanzania
Mbunge Cecil Mwambe - Tanzania

Mbunge wa Ndanda, Masasi, mkoa wa Mtwara, Cecil Mwambe amesema kuchelewa kulipwa wakulima haki yao ya mauzo ya korosho zao itakuwa na athari nyingi ikiwemo kuzuka njaa katika mikoa ya Mtwara na Lindi.

please wait

No media source currently available

0:00 0:05:51 0:00

Sikitiko la wakulima

Katika Mji wa Nanyamba, na Masasi Mtwara, kusini mwa Tanzania, wananchi wanaeleza kuwa kuchelewa kwa malipo ya korosho walizouza kunawaathiri pakubwa hasa katika msimu huu wa kuanza kwa masomo ya watoto wao.

please wait

No media source currently available

0:00 0:00:31 0:00

Shughuli ya ununuzi wa korosho inayofanywa na serikali nchini Tanzania bado inaendelea huku hali ya mambo ikionekana kuwa tata kutokana na uwepo wa malalamiko toka kwa wakulima hasa juu ya ucheleweshwaji wamalipo yao.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:05 0:00

Tamko la Waziri wa Kilimo

Waziri mwenye dhamana ya kusimamia Kilimo, Japhet Hasunga, anaeleza kuwa kuchelewa kwa malipo ya baadhi ya wakulima ni kutokana na uhakikina changamoto kadhaa ikiwemo kasoro katika taarifa za kibenk za wakulima.

please wait

No media source currently available

0:00 0:00:33 0:00

Kauli ya Waziri Mkuu

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa anasisitiza kuwashughuli ya uhakiki wa wakulima na mazao ni lazima ifanyike ili kuwabaini wanaojaribu kudanganya.

please wait

No media source currently available

0:00 0:00:31 0:00

Wasemavyo wataalam

Kwa mujibu wa taarifa ya timu ya wataalamu inayohusika na utekelezaji wa operesheni korosho zoezi la ubanguaji korosho linaweza kuchukua hadi miezi 14 kubangua korosho za msimu wa mwaka 2018/19 zinazofikia tani laki 2 na 75 elfu, na hii nikutokana na viwanda vingi kutofanya kazi hivi sasa.

Hata hivyo serikali nchini humo imechukuwa hatua ya kuwaita tena mezani wafanyabiashara wanaotaka kubangua korosho zilizokusanywa. Serikali imekaririwa na vyombo vya habari ikiwaalika tena wafanyabiashara wa korosho ambao wanataka kununua korosho na kuzibangua wenyewe kufanya hivyo

Serikali ya Tanzania ilitangaza mwaka 2018 mwishoni uamuzi wake wa kununua korosho kutoka kwa wakulima baada ya kuibuka mzozo wa ununuzi wa zao hilo kwa bei elekezi ya shilingi elfu tatu kwa kilo.

XS
SM
MD
LG