Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 17:54

Sadio Mane arejea tena mazoezini na  Bayern Munich


Mchezaji wa Senegal Sadio Mane akisherehekea baada ya mechi na Poland katika Uwanja wa Spartak, Moscow, Russia. REUTERS

Mchezaji Sadio Mane amerejea tena mazoezini na timu yake ya  Bayern Munich baada ya kuuguza jeraha la mguu lililomfanya nahodha huyo wa Senegal kukosa kushiriki michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

Mane alipata jeraha hilo wakati wa ushindi wa bao 6-1 dhidi ya Werder Bremen kwenye ligi ya Bundesliga tarehe 8 Novemba mwaka jana.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye alijiunga na Bayern kutoka Majogoo wa Uingereza Liverpool msimu uliopita wa joto, baadaye alifanyiwa upasuaji na kuunganishwa tena kwenye sehemu ya juu ya mshipa wake wa kulia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG