Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 17:07

SADC yapongeza uchaguzi wa DRC


Wapiga kura wakitafuta majina yao katika kituo cha kupigia kura Kinshasa
Wapiga kura wakitafuta majina yao katika kituo cha kupigia kura Kinshasa

Naibu mwenyekiti wa Sadc asema uchaguzi wa DRC ulifuata misingi ya kidemokrasi.

Mwakilishi wa jumuiya ya SADC ambaye pia ni msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania bwana John Tendwa amesema uchaguzi wa urais na bunge Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Ulifanyika kwa kufuata misingi ya kidemokrasi.

Amesema DRC nchi iliyogubikwa na ghasia za vita na matukio mengi ya ukiukwaji wa kibinadamu imeweza kuhamasisha watu kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura zao na kumchagua rais wa nchi yao.

Bwana Tendwa amekiri kuwa kulikuwepo na ghasia katika baadhi ya maeneo zilizosababishwa na kuchelewa kwa vifaa vya kupigia kura lakini hazikuweza kuvuruga uchaguzi huo.

Kuhusu wagombea wanne waliodai kufutwa uchaguzi huo kutokana na kutokuwa na misingi na kufuatwa utaratibu wa kupiga kura amewataka wagombea hao kwenda mahakamani kutoa malalamiko yao kama katiba inavyosema.

Aidha ameongeza kuwa utaratibu wa kumchagua rais ambaye amepata kura nyingi bila kujali kufikia kiwango Fulani cha kura umepokelewa sahihi na wagombea na wananchi wa DRC.

Rais Joseph Kabila ndiye anaongoza katika uchaguzi huo uliofanyika jumatatu hii.

XS
SM
MD
LG