Wizara ya mambo ya ndani ya Mexico imesema mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa zamanai wa Libya Moammar Gadhafi amekamatwa wakati akijaribu kuingia nchini humo kwa kutumia nyaraka za kugushi.
Pamoja naye watu wengine wanne wamekamatwa kuhusiana na njama hizo zilizofanyika mwezi novemba na kutangzwa jumatano.
Kukamatwa kwa wapangaji wa njama hizo zilizofanyika mwezi Novemba kulitangazwa jumatano.
Waziri wa mambo ya ndani wa Mexico Alejandro Poire amesema mpango ulikuwa ni kutoa nyaraka za kugushi kuonesha uraia wa Mexico kwa Saadi na familia yake na baadae kununua majengo kadhaa huko Mexico ambayo yatatumika kama hifadhi yao.
Moja ya nyumba zilizotarajiwa kununuliwa iko katika eneo la kifahari kwenye mji wa Bahia de Banderas katika jimbo la Nayarit.
Shirika la kijasusi la Mexico lilibaini kwa mara kwanza kuhusu mpango huo mwezi Septemba.
Aidha Poire anasema mawakala wa shirika hilo la kijasusi walifuatilia na kugundua kwamba Cynthia Ann Vanier raia wa Canada alikuwa kiongozi aliyewasiliana na familia ya Gadhafi na alikamatwa Novemba 10.