Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 29, 2022 Local time: 19:44

Saa zinayoyoma kujua serikali kuu Marekani itafungwa au la


Ikulu ya Marekani-White House

Huku wasi wasi ukiwa umetanda kuwa huenda serikali kuu ya Marekani ikafungwa kuanzia saa sita usiku wa Ijumaa, Rais wa Marekani Donald Trump ameakhirisha safari yake ya kwenda mapumzikoni huko Florida akisubiri baraza la seneti kuidhinisha mswaada wa muda wa matumizi ya fedha.

Rais Trump alipangiwa Jumamosi kuhudhuria harambee ya chakula cha usiku kuadhimisha mwaka mmoja wa urais wake lakini huku kukiwa na wasi wasi wa kuidhinishwa mswaada wa matumizi ya fedha na bunge, maafisa wa White House walisema rais ataendelea kuwepo Washington akisubiri suluhisho la bajeti ili kuepuka serikali kuu kufungwa.

Mkurugenzi ofisi ya utawala na bajeti, Mick Mulvaney
Mkurugenzi ofisi ya utawala na bajeti, Mick Mulvaney

Mkurugenzi wa ofisi ya utawala na bajeti Mick Mulvaney alisema Ijumaa nafasi ya kufungwa kwa serikali kuu ilikuwa “nusu kwa nusu” baada ya nafasi ya ushindi wa uungaji mkono wa kutosha kutoka Democrat kwa hatua iliyoonekana kupunguza makali ya kufungwa kwa serikali kuu.

“Tulikuwa tuna endesha shughuli chini ya kama asilimia 30 ya kufungwa kwa serikali kuu hadi Alhamis, ninafikiri hali imeongezeka hivi sasa” Mulvaney aliwaambia waandishi wa habari huko White House. “Tulikuwa na mkutano wetu kiasi cha nusu saa iliyopita, mkutano kwa njia ya simu na idara mbali mbali ili kuwaambia waanze kutekeleza mipango yao ya sera katika hatua ijayo ya kujiandaa na ukosefu wa fedha wakati serikali kuu inafungwa”.

Mkurugenzi wa bunge katika White House, Marc Short aliwaambia waandishi wa habari kwamba Rais Trump alipiga simu Ijumaa ili kujaribu kuzungumzia suala hilo lakini hakusema rais alimpigia nani. “Tunajaribu kuhakikisha serikali inaendelea kuwa wazi” alisema Short.

Jengo la bunge la Marekani, Washington DC Jan. 10, 2018.
Jengo la bunge la Marekani, Washington DC Jan. 10, 2018.

Mswaada uliopitishwa na bunge utaisaidia serikali kuwa wazi na kuendesha shughuli zake hadi Februari 16 lakini baraza la seneti lilimaliza siku bila ya upigaji kura hatua ambayo ingepelekea kuwasilisha hatua za muda za matumizi ofisini kwa rais.

Katika ujumbe alioandika Rais Trump Ijumaa asubuhi alikiri kwamba kura za Democrat zinahitajika kupitisha hatua hiyo lakini alipendekeza madai ya wademocrat ya kulinda suala la uhamiaji yataweza kuchelewesha fursa ya kupitisha mswaada huo na kupelekea serikali kuu kufungwa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG