Kiongozi wa mashtaka nchini Afrika ya Kusini amesema kuwa afisi yake ina mpango wa kukata rufaa kupinga kifungo cha miaka sita kilichotolewa na mahakama kwa mwanariadha Oscar Pistorius, na kudai kuwa mahakama haikutoa kifungo kilichostahiki.
Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka sita mapema mwezi huu baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp miaka mitatu iliyopita.
Kifungo hicho kilipunguza kutoka miaka kumi na mitano ambacho ndio muda mfupi sana unaotambuliwa na sheria za nchi hiyo. Katika kupunguza kifungo hicho, jaji Thokozile Masipa alisema kuwa mshtakiwa alionekana kuhuzunika na kuwa tayari alikuwa ametumika muda mrefu kwenye jela. Aliongeza kuwa Pistorius hakuwa amevaa mguu wake bandia wakati alipotekeleza mauaji hayo.