Vincent Karega balozi wa zamani wa Rwanda nchini Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako alifukuzwa Oktoba mwaka jana katikati ya mvutano kati ya nchi hizo mbili alichaguliwa na mamlaka mjini Kigali kuwa balozi nchini Ubelgiji.
Inasikitisha kwamba serikali ya Ubelgiji inaonekana kuwa imekubali shinikizo kutoka kwa serikali ya DRC na propaganda kutoka kwa mashirika na wanaharakati wanaopinga alisema msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo.
Hii haijakaa vyema kwa mahusiano ya pande mbili baina ya nchi zetu.
Forum