Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 11:42

Rwanda yashutumiwa na UN


Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame

Akizungumza katika mkutano mjini nairobi leo , waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikawabo amesema nchi yake imeomba ushahidi juu ya tuhuma hizo.

Rwanda imejibu ripoti ya wataalamu wa umoja wa mataifa iliyohusisha Kigali na uasi mashariki mwa DRC.

Akizungumza katika mkutano mjini nairobi leo , waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikawabo amesema nchi yake imeomba ushahidi juu ya tuhuma hizo.

Amesema nchi yake imetuma barua umoja wa mataifa kutaka maelezo juu ya tuhuma hizo za kulisaidia kundi la M23 nchini DRC. Anasema wamefanya majadiliano ya siku tatu na kundi hilo la wataalamu na kupitia kila tuhuma ambapo wametoa maeleo na nyaraka za uthibitisho za tuhuma za uongo

Waziri huyo amekiri kuwa haamini kama wataalamu wataweza kubadili mawazo yao lakini ilikuwa muhimu kwa Rwanda kujieleza juu ya suala hilo.
Ameongeza kuwa Rwanda imekosoa kuhusu ushahidi wa ripoti hiyo ya wataalamu wa UN ikiwemo picha za wanajeshi wa M23 waliovalia sare za jeshi la Rwanda. Ripoti hiyo pia imeripoti mazungumzo ya simu baina ya maafisa wa jeshi la Rwanda na wapiganaji wa M23.

Mushikawabo anasema mazungumzo hayo yalifanyika kabla ya uasi kuanza na walikuwa wanajaribu kushawishi wanajeshi kutojitenga.

Baadahi ya wafadhili wa wakubwa wa Rwanda wamejitoa kufuatia ripoti hiyo ya umoja wa mataifa.
XS
SM
MD
LG