Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 19:32

Rwanda: Wanahabari watatu waachiliwa huru baada ya kuzuiliwa jela kwa miaka minne


Rais wa Rwanda Paul Kagame

Mahakama moja nchini Rwanda Jumatano imewaachilia huru waandishi wa habari watatu ambao walikuwa wanazuiliwa jela kwa miaka minne kwa madai ya kueneza habari za uongo, kesi ambayo ilitajwa na makundi ya kutetea haki za binadamu kama uzushi.

Wanahabari hao watatu, Damascene Mutuyimana, Shadrack Niyonsenga na Jean Baptiste Nshimiyimana, walikamatwa mwezi Oktoba mwaka 2018 wakati wa msako mkali dhidi ya wakosoaji wa serikali ya Rais Paul Kagame wanaotumia mtandao wa Youtube.

Watatu hao walikuwa wanafanya kazi kwenye televisheni ya Iwacu inayopitisha matangazo yake kwa Youtube, na walishtakiwa kwa kuchochea uasi, kusambaza habari za uongo kwa nia ya kujenga hisia ya kimataifa ya uadui dhidi ya Rwanda na kuchapisha taarifa na picha za uongo.

Lakini mahakama ya mjini Kigali ya majaji watatu iliwafutia mashtaka yote, na kuamua kuwa waendesha mashtaka walishindwa kutoa ushahidi wa kutosha.

“Upande wa mashtaka ushahidi uliowasilisha haukutosha kwa uhalifu ambao washtakiwa hao watatu wanatuhumiwa. Lazima waachiliwe,” mahakama iliamua.

Wanahabari hao hawakuwepo mahakamani wakati wa uamuzi huo.

Wakili wao Jean Paul Ibambe ameiambia AFP kwamba amepokea kwa furaha kuachiliwa kwao.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG