Pato la taifa la Rwanda linatarajiwa kukua kwa asilimia 6.8 mwaka huu wa 2022, IMF imesema katika taarifa, ikiwa zaidi ya iliyotabiri mwezi Juni ambayo ilikua asilimia 6.
Makubaliano hayo ya ufadhili lazima yaidhinishwe na bodi ya uongozi ya IMF, ambayo imepanga kujadili juu ya makubaliano hayo mwezi Disemba mwaka huu.
IMF imesema ujumbe wake katika taifa hilo la Afrika mashariki ulijadili mageuzi ya kuimarisha mfumo wa fedha, kudumisha sera ya fedha yenye matarajio madhubuti na kupunguza athari za janga la Covid 19.
IMF imesema katika taarifa “Kushughulikia mfumko mkubwa wa bei, mahitaji ya maendeleo ya muda mrefu na hatari zinazojitokeza za hali ya hewa bado ni changamoto ya kisera katika mazingira tete ya kimataifa.”