Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 19:56

Rwanda inasema ndege ya vita ya DRC imeingia kwenye anga yake


Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame

Rwanda imesema ndege ya vita kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeingia kwenye anga yake Jumatano, huku mivutano kati ya majirani hao wawili ikiongezeka juu ya waasi wanaozidi kusonga mbele katika eneo lenye mzozo la mashariki mwa DRC.

DRC iliishtumu Rwanda kuliunga mkono kundi la waasi la M23, ambalo liliteka baadhi ya maeneo kutoka kwa jeshi la Congo na washirika wake wanamgambo katika miezi ya hivi karibuni.

Kigali ilikanusha madai hayo, ambayo yamethibitishwa na waatalamu wa Umoja wa Mataifa kadhalika na Marekani, Ufaransa na Ubelgiji.

Rwanda inaishtumu DRC kushirikiana na waasi wa FDLR, kundi la zamani la waasi wa Kihutu wa Rwanda lenye makao yake nchini DRC.

“Ndege ya vita aina ya Sukhoi 25 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilifanya ukiukaji na kuingia katika anga ya Rwanda kwenye Ziwa Kivu katika jimbo la magharibi nchini Rwanda nyakati za mchana,” serikali ya Rwanda imesema katika taarifa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa “ ndege hiyo ilirejea mara moja DRC.”

Tukio hilo linajiri chini ya miezi miwili baada ya Kigali kudai kwamba ndege nyingine ya vita ya DRC iliingia kwenye anga yake.

XS
SM
MD
LG