Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 23, 2023 Local time: 01:15

Rwanda inakabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei


Rais wa Rwanda Paul Kagame

Benki Kuu ya Rwanda imeongeza kiwango cha riba kutoka asilimia 6.5 hadi asilimia 7 kutokana na mfumuko wa bei.

Benki hiyo imesema kwamba kiwango cha mfumuko wa bei kilifikia asilimia 20.7 mwezi Januari.

Maafisa wamesema kwamba hawatarajii mfumuko wa bei kushuka hivi karibuni.

Hata hivyo, wanatarajiwa mfumuko wa bei kupungua hadi asilimia 8 ifikapo mwishoni mwa mwaka.

Wamesema kwamba vita vinavyoendelea Ukraine vimechangia katika kupanda kwa bei za bidhaa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG