Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 14, 2024 Local time: 11:16

Rwanda inajiandaa kuadhimisha miaka 30 ya mauaji ya Kimbari


Rais wa Rwanda Paul Kagame alipohutubia taifa wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 29 ya Mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 huko Kigali, tarehe 7 Aprili 2023. Picha na Mariam KONE / AFP.
Rais wa Rwanda Paul Kagame alipohutubia taifa wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 29 ya Mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 huko Kigali, tarehe 7 Aprili 2023. Picha na Mariam KONE / AFP.

Rwanda inajiandaa kuadhimisha miaka 30 ya kipindi cha kutisha zaidi katika historia ya taifa hilo ya mauaji ya halaiki dhidi ya Watutsi walio wachache.

Rwanda inajiandaa kuadhimisha miaka 30 ya kipindi cha kutisha zaidi katika historia ya taifa hilo ya mauaji ya halaiki dhidi ya Watutsi walio wachache. Hadi leo hii, makaburi mapya ya halaiki bado yanagunduliwa kote nchini humo kwenye watu milioni 14, jambo ambalo ni ukumbusho wa kusikitisha wa ukubwa wa mauaji hayo.

Wajumbe kutoka kote ulimwenguni watakusanyika Jumapili katika mji mkuu wa Kigali wakati Rwanda katika kumbukumbu za mauaji hayo ya mwaka 1994. Wageni mashuhuri wanatarajiwa kuwa ni pamoja na Bill Clinton, aliyekuwa rais wa Marekani wakati wa mauaji hayo ya halaiki, na Rais wa Israeli Isaac Herzog.

Katika video iliyorekodiwa kabla ya sherehe hizo, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema Alhamisi kwamba Ufaransa na washirika wake wangeweza kukomesha mauaji ya halaiki lakini hawakuwa na nia ya kufanya hivyo. Tamko la Macron lilikuja miaka mitatu baada ya kukiri jukumu kubwa la Ufaransa mshirika wa karibu wa Rwanda wa Ulaya mwaka 1994 kwa kushindwa kuzuia kuingia kwa nchi hiyo kwenye mauaji.

Forum

XS
SM
MD
LG