Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:10

Rwanda: Dereva aliyeua mwanahabari mashuhuri bila kukusudia apewa adhabu ya kulipa $920


Rais Paul Kagame
Rais Paul Kagame

Dereva mmoja raia wa Rwanda Jumanne alipewa adhabu ya kulipa faini ya faranga milioni moja za Rwanda, sawa na dola 920 kwa kuua bila kukusudia, kufuatia kifo cha mwanahabari mashuhuri ambaye alikuwa mkosoaji wa serikali.

John Williams Ntwali, muhariri wa gazeti la The Chronicles, aliuawa Januari 18 wakati gari lililokuwa likitembea kwa kasi lilipogonga pikipiki iliyokuwa inamsafirisha.

Mahakama ya mjini Kigali imesema dereva huyo, aliyetambulishwa kwa jina la Moise Emmanuel Bagirishya, “alikiri kosa na aliomba msamaha kwa ajali hiyo.”

“Alikiri kwamba alimuua Ntwali wakati alikuwa akiendesha gari kwa kasi na amechoka,” Jaji amesema, na amepatikana na hatia ya “kuua bila kukusudia na kusababisha hujuma ya mwili bila kukusudia.”

Kesi hiyo haikufuatiliwa na umma hadi Jumanne jioni wakati wanahabari wachache walipoalikwa kushuhudia kusomwa kwa hukumu hiyo.

Ntwali, ambaye alikamatwa mara nyingi katika miongo miwili ya kazi yake ya uandishi wa habari, alikuwa anamiliki televisheni ya Pax kwenye mtandao wa YouTube, ambayo ilikuwa imejidhihirisha kama chombo cha habari pekee kinachoripoti habari za kusimumua nchini Rwanda.

XS
SM
MD
LG