Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 02:29

Rwanda Burundi na Somalia zinadhimisha siku ya Uhuru


Wanawake wakihudhuria sherehe za uhuru wa Somalia mjini Mogadishu, Julai 1, 2012
Wanawake wakihudhuria sherehe za uhuru wa Somalia mjini Mogadishu, Julai 1, 2012

Kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya Miongo miwili wakazi wa Somalia washerehekea siku kuu ya Uhuru

Kwa miaka 21 ghasia na majanga ya kibinadamu yamegubika siku ya uhuru wa Somalia, lakini Julai 1 2012, mambo yalikuwa tofauti kabisa pale sherehe rasmi ziliweza kufanyika kutokana na kuimarika kwa usalama na utulivu.

Hali hiyo yote inatokana na juhudi za Jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika AMISOM, na majeshi ya Somalia kuwafukuza wanaharakati wa kundi la Al-shababkutoka mji mkuu huo.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika Mohammed Yusuf alihudhuria sherehe za uhuru mjini Mogadishu na kuripoti kwamba wakazi wanapumua hivi sasa lakini wasi wasi wao mkubwa ni jinsi uchaguzi mkuu utakavyofanyika hapo mwezi Ogusti mwaka huu.

Ahmed Afi, mfanyakazi wa shirika la msaada la Direct Aid lenye makao yake Kuwait anasema, ili amani na utulivu uweze kuendelea kutategemea na viongozi wa baadae wa nchi hiyo.

Nchini Rwanda kwa miaka 50, siku ya uhuru imekuwa ikisherekea kwa namna tofuati kwa kutegemea ni serikali ipi iliyo madarakani.Chini ya utawala wa Juvenal Habyarimana siku kuu ilikua inaadhimishwa Julai 4 siku ya mapinduzi.

Lakini, mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Kigali Sylvanus Karemera anaripoti kwamba baada ya mauwaji ya halaiki ya 1994 siku kuu imerudui kusherehekewa tarehe Mosi Julay chini ya utawala wa Rais paul Kagame.

Kwa wa Burundi miaka 50 ya uhuru inasherekewa kwa maoni yanayotafautiana, baadhi ya wananchi wanafurahia amani kwa wakati huu kukiwepo na maendeleo makubwa ya miundo mbinu na huduma za serikali. Wengine wanalalamika kwamba hakuna maendeleo makubwa kukiwepo baado na ukoesfu wa ustawi wa kisiasa na kijami.

Marekani imezipongeza Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na Somalia kwa kusherehekea siku kuu ya uhuru wao.

XS
SM
MD
LG