Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:06

Rutto: ICC imefuta kesi kwa vile hatukuwa na hatia


Naibu Rais wa Kenya, William Ruto akizungumza na waandishi wa habari kufuatia uamuzi wa ICC kufuta kesi iliyokuwa inamkabili.
Naibu Rais wa Kenya, William Ruto akizungumza na waandishi wa habari kufuatia uamuzi wa ICC kufuta kesi iliyokuwa inamkabili.

Naibu Rais wa Kenya, William Rutto amesema kutupiliwa mbali kwa kesi iliyokuwa inamkabili katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) kulitokana na yeye kutokuwa na hana hatia na si kinyume na hivyo.

Rutto alikuwa akiongea akiwa nyumbani kwake Karen mjini Nairobi na kusema kuwa kesi ya ICC dhidi yake na mwandishi wa habari Joshua Sang haikufutwa kwasababu ya mashahidi au wanasiasa bali ni kutokuwa kwao na hatia.

Amesema anawasamehe wote wale ambao waliamua kutoa ushuhuda wa uongo dhidi yao na kuongeza kwamba anawashukuru wote wale ambao wamekuwa wakiwaombea na kuwatia moyo katika kipindi chote kigumu wakati kesi hiyo ikiwa inaendelea.

Naibu Rais akiwa amekaa pamoja na mama yake Sarah na mkewe Racheal wakati akizungumzia kumalizika kwa kesi hiyo amesema kamwe serikali ya Jubilee haitapumzika mpaka muathirika wa mwisho wa ghasia za baada ya uchaguzi amehudumiwa na kuwashukuru waathirika hao kwa kuonyesha ushujaa wakati wa utaratibu wa kuwapatia makazi.

Naibu Rais alishtakiwa kwa kuhusika na vitendo vya kihalifu vya mauaji, kuhamisha watu kwa nguvu na kuteswa kwa watu wakati wa ghasia za uchaguzi mwaka 2007 and 2008. Sang naye alikabiliwa na mashtaka kama hayo.

XS
SM
MD
LG